Fasihi Kwa Ujumla

in Kidato I-IV/KIDATO V-VI

Maana ya Sanaa
Sanaa ni ufundi au ustadi wa kuwasilisha mawazo mbalimbali yaliyo katika fikra za binadamu.
Tanzu za Sanaa

FASIHI                          MUZIKI                         UCHORAJI
UDARIZI                       SANAA                         UFINYANZI
UCHONGAJI                USUSI                           MAONYESHO

FASIHI
Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Sanaa katika fasihi ni ufundi wa kutumia lugha ili kuleta hisia Fulani na kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
DHIMA ZA FASIHI
Kuelimisha jamii
Fasihi inapofikisha ujumbe wake kwa jamii juu ya kuepukana na vitendo vinavyoleta madhara katika jamii, kwa mfano kukataza jamii kutenda vitendo viovu kwa kupitia methali na misemo mbalimbali kwa mfano; asie sikia la mkuu huvunjika guu.

Kuburudisha jamii.
Fasihi pia hutumika kama kiburudisho, huleta furaha kwenye huzuni
kwa mfano; nyimbo, mashairi na maigizo hivi vyote kwa ujumla huburudisha jamii katika maeneo tofauti tofauti.

Kuunganisha watu wanaotumia lugha husika
Fasihi huunganisha watu maana wale wanaotumia lugha moja huunganishwa na aina ya fasihi inayotumia lugha yao kwani fasihi ni sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe wake. Kwa mfano nyimbo za Kiswahili huunganisha watu wanaozungumza Kiswahili.

Fasihi husisimua
Hii huonekana pale ambapo Fasihi inatumia misemo na tamathali za semi na picha kuelezea matukio mbalimbali aliotokea katika jamii husika, kwa mfano; “ndugu yetu amefariki”, “ametutupa mkono”, “ameaga dunia”.

Fasihi hukuza lugha ya jamii husika
Fasihi hukuza lugha kupitia namna tofauti tofauti ya jinsi inavyotumia lugha husika. Kwa mfano; kupitia muziki,mashairi, tenzi na ushauri lugha husika huongeza misamiati tofauti tofauti.

AINA ZA FASIHI
Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni;

  1. Fasihi similizi
  2. Fasihi andishi

Fasihi simulizi
Ni aina ya fasihi ambayo huifadhiwa kichwani na huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo.

Sifa za fasihi simulizi
Ni kongwe.
Ni mali ya jamii nzima.
Hukutanisha fanani na hadhira ana kwa ana.
Ina hali ya utendaji.
Hubadilika kutokana na mazingira.
Huwasilishwa kwa njia ya masimulizi.
Ina tanzu nyingi.
Ina wahusika wengi.

Fasihi andishi
Ni aina ya fasihi ambayo huhifadhiwa na kuwasilishwa kwa njia ya maandishi.
Kwa mfano; riwaya, tamthilia, na ushairi

Sifa za fasihi andishi
Si kongwe
Ni mali ya mwandishi au mtunzi
Haikutanishi fanani na hadhira
Haina hali ya utendaji hivyo si hai
Haibadiliki kutokana na mazingira
Ina tanzu chache
Ina wahusika wachache
Huwasilishwa na kuifadhiwa kwa njia ya maandishi

TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI
Fasihi simulizi                                                                                                        Fasihi andishi#000000 solid;margin:15px;width:95%;”>

Huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo Huwasilishwa na kuifadhiwa kwa njia ya maandishi
Ina tanzu nyingi  Kwa mfano;   ngonjera, maigizo, na methali Ina tanzu chache mfano; tamthilia na riwaya
Ni hai kwani huonesha vitendo Si hai haina vitendo
Ina wahusika wengi Ina wahusika wachache
Ni mali ya jamii nzima Ni mali ya mwandishi au mtunzi
Ni kongwe Si kongwe
Hukutanisha fanani na hadhira Haikutanishi fanani na hadhira

MCHORO WA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
FASIHI SIMULIZI

HADITHI             USHAIRI             SEMI          MAIGIZO
-Ngano                  -Mashairi              -Methali      -Vichekesho
-Tarihi                  -Nyimbo               -Misemo     -Majigambo
-Visasili                -Tenzi                   -Nahau        -Ngonjera
-Vigano                 -Ngonjera             -Mafumbo   -Michezo ya kuigiza
-Soga                                                 -Mizungu

  1. HADITHI

Ni tungo za fasihi za simulizi zitumiazo lugha ya nathari (maongezi ya kila siku) masimulizi huwa mafupi yaliyopangwa katika mtiririko wa visa na matukio.
Vipera vya hadithi

NGANO
Ni hadithi zitumiazo wahusika kama wanyama,miti au watu kueleza au kuonya kuhusu maisha na mara nyingi huishia kwa wahusika kuishi kwa raha mustarehe.

VISAKALE/TARIHI
Ni hadithi ambazo husimulia matukio ya kihistoria,matukio hayo huweza kuwa ya kweli au si ya kweli yaani ya kubuni na wahusika wake ni binadamu.

VISASILI
Ni hadithi ambazo hutumia wahusika kama miungu na binadamu na husimulia mambo yanayohusiana na maumbile  ya watu,wanyama,miti na vitu visivyo na uhai.

VIGANO
Ni hadithi zinazoeleza kuhusu makosa au maovu ya watu na kueleza maadili yanayofaa.

SOGA
Ni hadithi fupi za kukejeri na kuchekesha,wahusika wa soga ni wa kubuni

  1. USHAIRI

Ni tungo linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo kwa kutumia utaratibu maalum.
Shairi Ni utungo wenye mpangilio maalum wa silabi na lugha za mkato. Kuna mashairi ya kimapokeo yenye urari na mizani. Mizani ni idadi ya silabi zilizomo kwenye mstari wa shairi au utenzi katika shairi la kimapokeo, kila mstari mara nyingi hugawanywa nusu kwa nusu kwa idadi za mizani inayolingana.

Utenzi
Ni utungo mrefu wa kimasimulizi au mawaidha. Muundo wa utenzi hufuatana na shairi kwa kuwa ni mistari mifupi isiyozidi mizani kumi na miwili(12).Silabi za mwisho za kila mstari wa mwisho zinaweza kufanana katika utenzi mzma na zikifanana huitwa habari.

Nyimbo
Ni tungo zenye mpangilio maalum wa maneno na mahadhi yaani kupanda na kushuka kwa sauti.

Ngonjera
Ni aina ya muundo wa mashairi ya kimapokeo. Ngojera huwa katika muundo wa mazungumzo baina ya makundi mawili yanayolumbana au mjadala na baadaye kufikia muafaka kwa upande mmoja kukubaliwa na upande mwingine ,kwa njia hii ujumbe hutolewa kupitia malumbano kwa vile matatizo yote na kasoro kuhusu jambo linaloongelewa hutolewa.

  1. SEMI

Ni tungo za fasihi simulizi ambazo ni fupi zenye kutumia picha, tamathali za semi na ishara. Aghalabu ni mafunzo yanayokusudiwa kubeba maudhui yenye maana yanayofuatana ibara mbalimbali na matumizi.

Methari
Ni semi ambazo hutoa hekima na busara kwa jamii. Huundwa kwa mpangilio wa maneno unaoonesha pande mbili za fikra.                              Mfano;usipoziba ufa, utajenga ukuta
“Ngoja ngoja huumiza matumbo”

Nahau
Ni kauli zinazojengwa kwa picha kutumia maneno ya kawaida, ni semi zenye undani ambao wageni wasiojua lugha hiyo huambulia patupu.        Mfano; Kapata jiko- ameoa
Ana mkono mrefu- mwizi

Mafumbo
Ni kauli zinazoeleza maana waziwazi. Kauli hizi ambazo pia hutumia lugha ya picha hutolewa kwa uficho hivyo kuwafikirisha wasikilizaji na kupunguza watu watakaoelewa jambo lile

Vitendawili
Ni semi iliyofumbwa ambayo hutolewa kwa hadhira ili ufumbue. Kitendawili hufanya kazi ya kumfikilisha mfikiliaji, msikilizaji. Msikilizaji anapaswa kuvuta kumbukumbu zake ili kupata maana a kitendawili.

Mizungu
Ni kauli zenye picha za mafumbo na inaonesha ukinzani na fikra au tukio.  mizungu hutumika kwenye joga na miviga.

  1. MAIGIZO

Ni masimulizi yenye utendaji. Igizo huonyesha mambo yanayotokea katika jamii. Maigizo hufanyika jukwaani au uwanjani. Lengo ni kufikisha ujumbe kwa usimulizi na vitendo.

Michezo
Maigizo yenye visa virefu vinavyoakisi maisha fulani ya jamii. Maudhui ya michezo inachambua mambo kwa undani na kuyatolea maoni.

Vichekesho
Ni maigizo mafupi yanayokusudiwa kufundisha na kuchekesha hadhira. Kwa kawaida vichekesho huonesha tu jambo au tatizo kwa njia ya uchekeshaji bila kulichambua kwa kina.

Majigambo
Ni maigizo ya kujigamba kwa kufanya jambo la kishujaa lisilo la kawaida mtendaji anasimulia na kutenda akionesha jinsi alivyofanya jambo lile.

Ngonjera
Ni maigizo yenye kutumia mashairi. Waigizaji wanawasiliana kwa kueleza mambo wakitumia beti za mashairi.

UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Uhakikiwa kazi za fasihi simulizi ni kitendo cha kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo.                     Au
Ni kitendo cha kuchunguza kazi ya fasihi ili kubaini ubora au udhaifu wake katika maumbo ya fani na maudhui.

UMUHIMU WA UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Kupata na kujua ufafanuzi wa kimaudhui wa kazi ya fasihi.
Kuchambua au kufafanua picha za kisanii zinazotumika katika kazi ya fasihi.
Itasaidia kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi ya fasihi.
Kukuza kazi za fasihi simulizi.